Coaches Across Continents
Name: | Coaches Across Continents |
---|---|
City: | Watertown |
Country: | United States of America |
Membership: | Adult Member |
Sport: | Football/Soccer |
© Copyright 2022 Sport Session Planner Ltd.
Developed with Partnership Developers, a division of Kyosei Systems.
Animation Controls (PCs, Macs, Laptops):
Play animation
Play step-by-step
Repeat (toggle)
Full Screen
Pause
Stop
Back/Forward: Drag timeline button
#9 Tumia bidhaa zinazotunza Mazingira (30 mins)
Mchezo wa Kukusudia
Gawa wachezaji kwa timu mbili. Uwe mchezo wa kutumia dakika 7 kila mkondo (Badilisha muda au idadi kulingana na muda ulioko)
Kila timu ina magoli 2 ya kufungia. Goli moja linawakilisha mahali ambapo wanaweza kuyapata matunda na mboga, wachezaji wakifunga kwa goli lile dakika 1 inaongezwa timu hiyo na wanapokea kiduta cha pia chenye rangi ya kijani.
Goli la pili linawakilisha coca cola au vyakula Fulani vya kigeni “Wanavyopenda”. Wakifungia humu timu inapoteza dakika 1 ya kucheza na wanapokezwa kiduta cha pia chenye rangi nyekundu.
Cheza na huku ukifuatilia maamuzi.
Maswali ya kukusudia wakati mchezo unaendelea - Uliza maswali na utegee majibu
Je? bidhaa zinazotunza mazingira zinamaanisha nini kwako? Umeshawahi lifikiria hili?
Unadhani ni kwa nini tuliuondoa muda/ kupunguza muda kutoka kwa kitengo cha vyakula vinavyoagizwa kutoka ng’ambo?
Kwa nini haifai vyakula kukaa njiani kwa muda mrefu kabla havijawafikia watumiaji?
Mchezo wa kukusudia- Tumia ubunifu wako au unaweza kuutumia huu tulioupendekeza ili uunde njia mpya za kuucheza.
Cheza tena lakini sasa uliza wachezaji kama kuna sehemu nchini mwao ambazo wanajua kuwa zina vyakula bora vya humuhumu ambavyo vinaweza kuliwa badala ya kutumia vile vya kigeni hasa (mchele na viazi mbatata vya kupika chipsi na vilevile nafaka nzuri)
Wape wachezaji au timu sekunde 30 za kuweka mikakati yao.
Ujumbe ulioko hapa kwenye mchezo ni bidhaa zinazoletwa kutoka mbali hutumia kiwango kikubwa cha kawi hivyo huongeza kiwango kikubwa cha kaboni kwenye hewa
Maswali ya kukusudia baada ya mchezo - Uliza maswali na utegee majibu.
Je? Ni zipi bidhaa za vyakula unavyovipenda kutoka humuhumu nchini au hata mashinani?
Je? Ni lipi ambalo ni jukumu lako la kuweza kuchagua vyakula vinavyotunza viwango vya hewa nzuri katika mazingira?
Ni yapi manufaa yatakayokuwepo ikiwa utanunua bidhaa zinazozalishwa mashinani?
Ni kipi tunachoweza kukifanya ili kutunza hewa ya mazingira/kupunguza kaboni?