Coaches Across Continents
Nombre: | Coaches Across Continents |
---|---|
Ciudad: | Watertown |
País: | United States of America |
Deporte: | Fútbol |
© Copyright 2022 Sport Session Planner Ltd.
Desarrollado con Partnership Developers, una división de Kyosei Systems.
Por favor, escoge de las siguientes opciones cómo te gustaría que presentara tu sesión.
Controles de la Animación (PCs, Macs, Portátiles):
Reproducir animación
Reproducir paso a paso
Activar/Desactivar Repetición
Pantalla Completa
Pausa
Detener
Atrás/Adelante: Deslizar el botón de línea de tiempo
#10 SEMA KWA SAUTI/SEMA USIKIKE
Mchezo wa Kukusudia
Thuluthi moja ya wachezaji wawe ndani ya duara na bila mpira na waliosalia waunde duara huku wengine wao wakiwa bila au wakiwa na mpira.
Mchezaji aliye ndani ya mduara aagizie mpira kutoka kwa mchezaji aliye nje na mpira halafu arejeshe mpira hadi katikati na aupitishe kwa mchezaji asiyekuwa na mpira
Washiriki ni lazima warudi kwa kiduta kilicho katikati kabla ya kuendea mpira mwingine.
Wachezaji wanaweza tu kubadilishana nafasi baada ya sekunde thelathini za shughuli. Wachezaji wakumbushwe kuwa lazima waite kwa sauti ndipo wapewe “mpira”
Maswali ya Kusudi wanapokuwa wakicheza -uliza maswali na utegee majibu.
Ni Kipi kilitokea ulipoendea mpira kimya kimya? Ingekuwa vipi ukilinganisha na kupaza sauti?
Je, ni rahisi kusema kwa sauti kuu?
Ni Kipi kinachowazuia watu kupaza sauti na kuchukua hatua maalum?
Mchezo wa kukusudia – Tumia ubunifu wako au pendekezo letu ili kubuni njia mbadala za kuucheza
Cheza kwa kubadilishana au kupokezana, badala kutaja “mpira” mchezaji wa katikati ataje mmea au mnyama ampendaye.
Pokezana tena na sasa mchezaji wa katikati ataje kwa sauti mazingira au makazi ambayo anawazia kulinda au kuhifadhi.
Ya mwisho sasa mchezaji mmoja wa katikati ataje kwa sauti maamuzi au hatua ambayo atachukua ili kuhifadhi makao ya mnyama au mmea au mazingira.
Kwa kila mguso wa mpira wawe wakibadilisha ni sehemu gani ya mwili itapokea na kusongesha mpira kwa mchezaji wa katikati.
Maswali ya kukusudia baada ya mchezo- Uliza maswali na utegee majibu
Ni kipi kitatokea iwapo hakutakuwepo na hali nzuri ya kusema kwa kupaza sauti?
Je ulihisi vipi ulivyoweza kujisemea kwa sauti kuu kabla ya kupokea mpira?